Kabla ya kuuza hadithi zao kwenye programu ya simulizi, mtunzi wa Simulizi anapaswa kukubaliana na sheria na masharti yafuatayo ili kudumisha viwango vya ubora, haki za kisheria, na maadili kwenye App hii. Zifuatazo ni baadhi ya sheria hizo: 1. Haki ya Hakimiliki na Umiliki: - Unakubali ya kwamba wewe ni mtunzi au unamiliki hadithi zote unazouza ndani ya App hii. - Zingatia ya kwamba hatutahusika endapo utauza hadithi ambazo huna umiliki nazo. 2. Maadili na Vigezo: - Hadithi zinapaswa kuzingatia maadili na sheria zinazotambulika kuhusu lugha, maudhui, na picha zinazoweza kuathiri watoto au kundi lolote la jamii. - Zingatia ya kwamba unapaswa kutoa taarifa juu ya makundi ya watu kwa umri wanaopaswa kusoma au kusikiliza hadithi husika. 3. Usalama wa Mtandao na Takwimu Binafsi: - Unapaswa kuhakikisha kuwa taarifa utakazo toa ni za kweli ili kuzuia matumizi mabaya ya takwimu binafsi za watu wengine. Hizi ni sheria chache ambaz...